Wednesday, 31 May 2017

LEMA AHOJI ALIKO YERIKO NYERERE

Tokeo la picha la yeriko nyerere

Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema) Godbless Lema ameuliza swali je, Yeriko Nyerere amekamatwa au ametekwa? Lema ameuliza swali hilo katika mtandao wake wa Twitter leo na kuongeza: “Msiogope. Lakini kwa kadiri ya walivyowatesa ndivyo walivyoongezeka na kuzidi kuenea."

Yeriko anayefahamika kuwa ni kada wa Chadema, amekamatwa leo saa tisa alfajiri na watu wanaodhaniwa kuwa ni polisi akiwa nyumbani kwake, Kigamboni, Mbutu.

Meya wa Ubungo, Boniphace Jacob amethibitisha kukamatwa kwa Yeriko.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment