Wednesday, 31 May 2017

FAGIO LA VYETI FEKI LAATHIRI IDARA YA AFYA NA ELIMU, CHALINZE

unnamed

HALMASHAURI ya Chalinze,Bagamoyo ,mkoani Pwani imeiomba serikali kupeleka watumishi katika idara ya afya na elimu ,mara baada ya utaratibu wa uhakiki kukamilika ili kuziba pengo la watumishi 42 waliokumbwa na adha ya vyeti feki.

Aidha halmashauri hiyo imefanikiwa kutimiza malengo yake sita ndani ya kipindi cha miezi Tisa ,ikiwemo kuinua mapato yake ya ndani.

Hayo yaliyasemwa na mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Said Zikatimu alipokuwa akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani huko Lugoba .


Alielezea kuwa wameinua mapato hayo kutoka kiasi cha Sh mil 130 hadi kufikia Sh Mil  390 sawa na asilimia 120 kwa mwezi na kuwa ya kwanza kimkoa.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment