Wednesday, 17 May 2017

DAR KUANZA UJENZI WA VITUO VYA MABASI YA MIKOANI

Tokeo la picha la SELEMANI JAFO

Serikali kwa kushirikiana na Halmashauri ya jiji la Dar es salaam wanatarajia kuanza ujenzi wa vituo vipya vya mabasi yaendayo mikoani na Nchi jirani.

Hayo yamesemwa leo bungeni Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge.

Selemani Jafo amesema kuwa vituo hivyo vya mabasi ni vya mikoa ya Kanda ya Kaskazini, Nyanda za juu Kusini, kanda ya Magharibi, kanda ya Ziwa, kanda ya Kati, na Nchi jirani za Kenya, Uganda, Malawi, Burundi, Rwanda na Zimbabwe.


 Aidha ameongeza kuwa lengo kuu ni kuhakikisha vituo hivyo vinajengwa na kuwasaidia wananchi kupata usafiri mzuri.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment