Wednesday, 17 May 2017

CHADEMA WATAKA WALIOATHIRIWA NA CDA WALIPWE FIDIA

Tokeo la picha la Benson Kigaila

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kati kimeitaka serikali kuwalipa fidia wakazi wa Manispaa ya Dodoma ambao kwa namna moja au nyingine wameathirika wakati Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) ilipokuwa ikifanya kazi kwa kuporwa ardhi yao.

Mkurugenzi wa Mafunzo na Oganaizesheni wa Chadema, Benson Kigaila amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Dodoma na kudai kuwa Rais, Dkt. John Magufuli hawezi kuivunja CDA na ikawa ndiyo mwisho wake bila kuangalia madhara yaliyosababishwa na mamlaka hiyo kwa wananchi katika kipindi chote cha miaka 44 iliyofanya kazi.

Amesema fidia hiyo ni lazima ilipwe na serikali kuu ambayo ndiyo iliyoiweka CDA madarakani na siyo kuliachia jukumu hilo Manispaa ya Dodoma kwa kuwa haihusiki na unyang’anyi huo.

 “Kuivunja CDA siyo hoja. Hoja inayokuja hapo ni je wananchi wa Dodoma walionyang’anywa ardhi yao na CDA bila kulipwa fidia watafidiwaje au ndiyo wataachwa waendelee na maumivu yao?,” amehoji Kigaila.


 Hivi karibuni Rais Magufuli aliamua kuivunjilia mbali Mamlaka ya CDA na kusisitiza kuwa waliokuwa wafanyakazi wake wataendelea na kazi katika maeneo mengine watakayopangiwa.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment