Friday, 19 May 2017

BIDHAA FEKI KUWANG'OA WATUMISHI

Tokeo la picha la charles mwijage

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage amesema watumishi wa umma watakaoruhusu bidhaa feki kuingia kwenye soko la ndani wajiandae kuachia nafasi zao.

Mwijage ametoa onyo hilo juzi Bungeni mjini Dodoma, wakati akisoma bajeti ya wizara yake, ambapo pia alipiga marufuku bidhaa bandia kuingia nchini kutoka nje ya nchi kuanzia Julai mosi mwaka huu.

“Ikifika mwezi Julai mwaka huu, kama bidhaa feki zikipita kuingia nchini mtakuwa hamnitakii mema, na walio chini yangu mkae kabisa mkao wa kuondoka kama bidhaa zisizokidhi viwango zitapia na kuja kuumiza viwanda vyetu nchini,” alisema.

Aidha,viwanda vingi nchini vimepunguza uzalishaji kutokana na ukweli kuwa takwimu zinaonyesha kuwa mwaka jana Tanzania iliuza bidha za viwanda zenye thamani ya dola za Marekani bilioni 1.4 ambapo pia takwimu za mwaka huu zinaonyesha mauzo ya bidhaa nje ya nchi yameshuka kwa dola za Marekani milioni 500.


Uingizwaji wa bidhaa feki ume endelea kuwa kero kubwa kwa wananchi ikiwemo kupoteza fedha na kutokea majanga kutokana na vitu hivyo ikiwemo vifaa vya kielektroniki kulipuka.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment