Friday, 28 April 2017

WENYE VYETI FEKI WATUMBULIWARais Magufuli 

Rais Dk John Pombe Magufuli leo amatangaza kuwafuta kazi watumishi 9732 wenye vyeti feki kufuatia uhakiki ulifanyika kwa muda wa miezi kadhaa na kumtaka Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kutangaza nafasi za kazi ili kuziba nafasi za watumishi walioondolewa.

Akizungumza wakati akipokea Ripoti ya Vyeti feki leo mjini Dodoma Rais Magufuli amesema taifa haliwezi kuendelea kuwa na wafanyakazi wenye vyeti feki kwa sababu hawatakuwa na ufanisi katika nafasi zao za kazi.

Amesema Watumishi wenye vyeti feki ambao idadi yao inafikia 9732 kuanzia leo waondolewe kwenye nafasi zao za kazi na mshahara wao ukatwe mara moja pamoja.


Alisema watakaojiondoa wenyewe kazini kabla ya Mei 15, mwaka huu hawatashitakiwa, watakaokaidi baada ya hapo watafikishwa mahakamani.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment