Monday, 24 April 2017

UVCCM YAPANGA SAFU MPYA YA UONGOZI

7ulsz52Q
U
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) leo umetangaza safu mpya ya viongozi katika idara mbalimbali ndani ya umoja huo.

Akitangaza safu hiyo, Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka, amesema idara zimeongezwa kutoka nne hadi kufikia tano.

Amewataja waliopitishwa pamoja na idara zao katika mabano kuwa ni pamoja na Jokate Mwegelo (Uhamashishaji na Chipukizi), Dorice Obed (Uchumi, Uwezeshaji na Fedha), Daniel Zenda (Vyuo Vikuu), Israel Sostenes (Usalama na Maadili) na Mohamed Abdalla (Oganaizesheni, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa).

Shaka amewataka vijana wote nchini kuendelea kulinda Muungano ambao Aprili 26, mwaka huu utakuwa unafikisha miaka 53 tangu kuzaliwa kwake.


“Hii ni tunu kubwa sana kwa Taifa letu hivyo vijana tuna wajibu wa kuulinda Muungano na kufanya kila linalowezekana kuhakikisha amani na utulivu vinaendelea kutawala,” amesema Shaka.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment