Friday, 28 April 2017

TRUMP AIONYA TENA KOREA KASKAZINI

Rais wa Marekani Donald Trump.

Rais wa Marekani, Donald Trump ameonya kwa mara nyingine tena kwamba mzozo mkubwa utaibuka dhidi ya Korea Kaskazini kuhusu mpango wake wa kinyuklia na ule wa kutengeza makombora.

Katika mahojiano na chombo cha habari cha Reuters, Trump amesema kuwa angependelea mzozo huo kukabiliwa kidiplomasia lakini amesema hiyo itakuwa vigumu kutimizwa.

Aidha, Trump amempongeza Rais mwenzake wa China, Xi Jinping akisema kuwa amekuwa akijaribu kwa kila njia kuishinikiza Korea Kaskazini kuachana na mipango yake ya kinyuklia.

Awali Waziri wa Maswala ya Kigeni nchini Marekani, Rex Tillerson alisema China imeionya Pyongyang kuwa itarajie vikwazo iwapo itafanya majaribio mengine ya kinyuklia.


Wakati huohuo Korea Kaskazini imetoa kanda ya video ya propaganda ikionyesha itakavyoishambulia Marekani. Kanda hiyo inahusisha Ikulu ya Whitehouse na ndege ya kubeba ndege za kijeshi na ikulu hiyo ikilipuka.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment