Friday, 28 April 2017

SABA WATIWA MBARONI VURUGU KATIKA MKUTANO WA CUF


Watu saba akiwemo mfuasi wa Profesa Ibrahim Lipumba, Abdul Kambaya wamekamatwa kwa kusababisha vurugu katika mkutano wa Chama cha Wananchi (CUF) uliofanyika hivi karibuni.

Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema hayo leo na kudai kuwa upelelezi wa sakata hilo umekamilika na tayari jalada la mashtaka dhidi ya watuhumiwa hao lipo kwa Wakili wa Serikali.


Kambaya ni Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa CUF ya Profesa Lipumba na hivi karibuni alikiri upande huo kutuma watu hao wanaodaiwa kufanya fujo katika mkutano huo huku wakiwa na silaha za jadi na moto kwa madai ya kufanya doria.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment