Monday, 24 April 2017

POLISI WAZUIA MKUTANO WA MBUNGE WA TEMEKE NA MAALIM SEIFKatibu mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad


Jeshi la Polisi Dar es Salaam limezuia kikao cha Mbunge wa Temeke (CUF) Abdallah Mtolea, ambao ulipangwa kufanyika leo kutokana na sababu zisizofahamika.

Mtolea alithibitisha hapo jana kufanyika kwa kikao hicho ambapo mkutano huo ulitarajiwa kuhudhuriwa na Katibu Mkuu CUF, Maalim Seif Sharif Hamad.

Aidha, alidai kuwa lengo la kikao hicho ni kufanya harambee za kuchangisha fedha kwa ajili ujenzi miundombinu ya eneo la Kilakala hasa wakati wa mvua.

 “Taarifa nilizopata kutoka polisi zinadai kuwa nilipanga kuwakusanya wafuasi wa lipumba na kuwashawishi kuhamia kwa Maalim kitu ambacho si cha kweli,” amesema Mtulia.

Zuio hilo linakuja siku chache ikiwa Juzi Aprili 22, mwaka huu, watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahimu Lipumba, walivamia mkutano wa wafuasi wa Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad na kuwapiga na kuwajeruhi wenzao pamoja na waandishi wa habari.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment