Tuesday, 25 April 2017

NEWCASTLE UNITED YAREJEA LIGI KUU ENGLAND

Tokeo la picha la newcastle united back to premier league

Klabu ya Newcastle United chini ya Kocha Rafa Benitez, itakipiga katika Ligi Kuu ya England msimu ujao baada ya kupanda tena daraja kutoka Championship kwa kuichapa timu ya Preston kwa mabao 4­1.

Mshambuliaji wa Newcaste Ayoze Perez ndiye aliyeanza kuiandika timu yake goli la kuongoza katika dakika ya saba ya mchezo lakini Preston wakachomoa goli hilo dakika ya kumi na nne kupitia kwa mshambuliaji wake Jordan Hugill.

Kiungo Christian Atsu akaiongezea Newcastle bao la pili katika dakika ya arobaini na tano ya kipindi cha kwanza kabla ya winga Matt Ritchie kuongeza bao la tatu dakika ya sitini na tano kwa vijana wa Rafa Benitez kwa mkwaju wa penati.


Mshambuliaji Ayoze Perez akashindilia msumari wa mwisho dakika chache baadae na kuwahakishia Newcastle kurejea tena katika ligi kuu msimu ujao.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment