Monday, 24 April 2017

MSEMAJI WA UPINZANI ASUSA KUSOMA HOTUBA YAKE

Tokeo la picha la Musa Zungu

Hotuba ya Upinzani imekwama kusomwa Bungeni na Msemaji wa upinzani katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano, Ally Salehe katika kikao cha kumi na moja cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 mjini Dodoma leo.

Mbunge Alli Salehe alisusia hotuba yake hiyo baada ya kulazimishwa kuacha kusoma baadhi ya maneno yakiwamo yanayohusu Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar na mgogoro wa CUF unaoendelea kutikisa kwa sasa.

Maneno mengine ni “Kila wizara imekiona cha moto, wamebanwa mpaka wamevunjwa mbavu” na kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais imeathirika vibaya na kisu cha ngariba kwa kukata bajeti yake.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG), George Masaju amepinga baadhi ya maneno aliyotumia Mbunge huyo hivyo kuzua malumbano.

Kufuatia Malumbano hayo Mwenyekiti wa Bunge, Musa Zungu alitoa uamuzi kuwa maneno yaliyoandikwa kuanzia ukurasa wa tatu hadi wa saba kwenye hotuba hiyo yasisomwe wala kurekodiwa kwenye kumbukumbu rasmi za Bunge.

Kutokana na malumbano hayo yaliyomtaka msomaji kufuta maneno ya kwenye Hotuba hiyo Mbunge huyo wa CUF alisema hawezi kuisoma hotuba yake bila hayo maneno.


“ Siwezi kuendelea kuisoma hotuba yangu na yaliyobaki namwachia ngariba afanye anavyotaka”Alisema Salehe

Reactions:

0 comments:

Post a Comment