Saturday, 15 April 2017

KUFA KUFAANA YAMRUDISHA BUNGENI MCHUNGAJI LWAKATARE

Tokeo la picha la mama lwakatare

Mchungaji wa Kanisa la Assemblies of God, Mikocheni B, Jijini Dar es Salaam, Getrude Rwakatare amechaguliwa kuwa Mbunge wa Viti Maalum ili kujaza nafasi iliyoachwa na kada aliyetimuliwa uanachama, Sophia Simba.

Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Ramadhan Kailima amesema kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kilipeleka jina la Mchungaji Rwakatare ambapo walipitia fomu zake na kuridhika kuwa mteule huyo ana sifa za kuwa mbunge.


Machi 11, mwaka huu, Sophia Simba ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) alitimuliwa uanachama kwa madai ya ukiukwaji wa maadili ya chama hicho na hivyo kumfanya kukosa sifa ya kuendelea kuwa mbunge kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment