Monday, 24 April 2017

GERALD MILLER AWATOA NISHAI VIJANA MASHINDANO YA MAGARI IRINGAMKIMBIZA magari mkongwe toka Arusha, Gerald Miller ameibuka mshindi katika mashindano ya mbio za magari Iringa zilizodhaminiwa na kiwanda kipya cha Maji Mkwawa cha mjini Iringa.

Pamoja na Miller, mshindi wa pili na wa tatu walioshinda mashindano hayo ya umbali wa zaidi ya kilometa 300 walikuwa walikuwa wakitumia magari aina ya Mistubishi Evo IX.

Matumaini ya mkurugenzi wa kiwanda hicho cha maji, Ahamed Huwel aliyekuwa akitumia gari mpya aina ya Ford Proto hayakuzaa matunda baada ya gari hiyo kupata hitilafu iliyompotezea zaidi ya nusu saa katika matengenezo yake.


Huwel aliyekuwa akipewa nafasi kubwa ya kuibuka mshindi kutokana na umaridadi wa gari yake, aliambulia nafasi ya saba kati ya washiriki kumi waliosalia katika mashindano hayo yaliyoshirikisha madereva 14.

Mashindano hayo yaliyofanyika kwa siku mbili (April 22 hadi 23) yalishuhudiwa ushindani mkali miongoni mwa washiriki, lakini Miller akiwa na msoma ramani wake Peter Fox wakitumia gari ya aina ya Mistubishi Evo IX waliibuka kidedea.

Nafasi ya pili katika mashindano hayo ilikwenda kwa Randeep Singh na msoma ramani wake Zubayr Piredina waliotumia pia gari aina ya Mistubishi Evo IX huku nafasi ya tatu ikienda kwa Dharam Pandya na msoma ramani wake Awadh Bafadhi waliotumia pia Mistubishi Evo IX.
Davis Mosha aliyewahi kuwa Makamu wa Rais wa Klabu ya Yanga, alishika nafasi ya nane yanayotarajia kufanyika kwa mara nyingine mwakani kwa udhamini wa Maji Mkwawa.

Wengine walioshiriki na nafasi zao kwenye mabano ni ni Sammer Nadhi (4), Deer Harinder Moses (5), Gurpal Sandhu (6), Hamid Mbata (9) na Frank Tayloe (10).

Walioshia katikati ya mashindano hayo baada ya magari yao kupata hitilafu nmi Kevin Taylor, Preetam Gandamal, Issack Taylor na Cyprian Mwaimu.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza alikabidhi zawadi ya vikombe kwa washindi na washiriki wote wa mashindano hayo katika hafla iliyofanyika nje ya kiwanda cha Maji Mkwawa.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment