Thursday, 20 April 2017

DK MAGUFULI MGENI RASMI SHEREHE ZA MUUNGANO

Tokeo la picha la John Magufuli

Serikali kuptia Waziri mkuu Kassim Majaliwa imesema kuwa mpaka sasa jumla ya watumishi wa Serikali 2,066 wametekeleza agizo la serikali la kuhamia Dodoma kutoka Dar es salaam.

Majaliwa ameyasema hayo jana katika viwanja vya mashujaa mkoani humo wakati akifungua maonyesho yaliyoandaliwa na baraza la taifa la uwezeshaji wa wananchi kiuchumi (NEEC).

Majaliwa alisema azma ya serikali kuhamia Dodoma ilitangazwa katika viwanja hivyo na rais Dk. John Magufuli.

Wakati huohuo Majaliwa amesema kuwa april 26 mwaka huu maadhimisho ya Muungano wa Tanganyika na zanzibar yatakuwa mkoani Dodoma ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Magufuli.

Majaliwa amesema maadhimisho hayo ya Muungano yanatarajiwa kufanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.


Licha ya Maadhimisho ya Muungano,lakini pia Sikukuu ya Wafanyakazi (Meimosi) itafanyika pia mkoani Dodoma katika uwanja huo huo wa Jamhuri

Reactions:

0 comments:

Post a Comment