Thursday, 16 March 2017

WAZIRI WA AFYA ATOA MAAGIZO MAZITO MKOANI IRINGA

UMYYYYYYYYYYYYYYY

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ameagiza kuanzishwa duka la Dawa ndani ya miezi 3 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa.

Aliyasema hayo mjini Iringa leo, katika ziara yake aliyofanya katika hospitali ya mkoa wa Iringa alikotembelea Kituo cha Damu Salama na kisha baadaye kwenda mjini Mafinga, wilayani Mufindi alikotembelea Hospitali ya Wilaya ya Mufindi, mjini Mafinga.

Pia naagiza Uongozi wa  Hospitali zote za Mikoa na Wilaya kuanzisha Wodi za Watoto Wachanga na Watoto Njiti mara moja.

Mbali na hayo Waziri Ummy  ameagiza kujengwa kwa  Kitengo cha Wagonjwa wa Dharura (Emergency Unit) kwa hospitali hizo mara moja ili kuboresha huduma ya afya kwa wakazi wa Iringa.

Akitoa taarifa ya utoaji wa huduma za Afya katika mkoa mbele ya Waziri wa Afya, mhe. Amina Masenza, mkuu wa Mkoa wa Iringa alieleza hatua mbalimbali wanazochukua katika kuboresha utoaji wa huduma ikiwemo kuboresha miundombinu ya vituo vya Afya, upatikanaji wa dawa, vifaa na vifaa tiba, utoaji wa elimu ya uzazi wa mpango pamoja na lishe kwa wananchi bila kusahau kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).

Hata hivyo, zipo changamoto kadhaa zinazowakabili mkoa kufikia lengo la lao kutoa huduma bora za Afya. Mathalani katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Iringa haina wodi/kitengo cha dharura, upungufu wa watumishi, Ufinyu wa eneo la Hospitali, ukosefu wa Gari la Kubebea Wagonjwa na ukosefu wa baadhi ya vitendanishi.

Mwalimu amewapongeza viongozi na watumishi wa mkoa kwa juhudi kubwa wanazofanya katika kuboresha huduma za afya ikiwemo kufanikisha ujenzi wa wodi ya watoto waliozaliwa kabla ya wakati na watoto wachanga.

Wodi hiyo yenye vifaa vyote muhimu imejengwa kwa ufadhili wa Kampuni ya ASAS ya Mjini Iringa.


Mwalimu amewataka wadau wengine waendelee kusaidia sekta hii hususani eneo la Afya ya Mama na Mtoto kwa kuwa linawagusa wananchi wengi hasa wa kipato cha chini.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment