Friday, 17 March 2017

TUNDU LISSU ATUA ARUSHA TAYARI KWA UCHAGUZI MKUU WA TLS

Tokeo la picha la Tundu Lissu atua arusha

MBUNGE wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema)anayewania Urais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) amekwea pipa na kutoa jijiji Arusha jioni ya leo baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo (Ijumaa) kumuachia, kwa dhamana ya bondi ya Sh10 milioni.

Lissu amedhaminiwa na maelezo ya awali yatasomwa Aprili3, mwaka huu. Leo asubuhi, Lissu alisomewa mashtaka matano na Wakili wa Serikali, Faraja Nchimbi likiwamo ya kutoa maneno yenye nia ya kuhimiza hisia za kidini ambayo yangeweza kupelekea uhasama baina ya jamii za Watanzania.

Lissu ambaye anajiwakilisha yeye mwenyewe mahakamani hapo aliomba maelezo hayo ya awali yasomwe Jumatatu, ili aweze kuhudhuria uchaguzi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) unaotarajia kufanyika kesho.


Taarifa zilizoufikia mtandao huu jioni hii zinaonesha mgombea mwenzake wa nafasi hiyo, Lawrance Masha amejitoa na amewataka wapiga kura wake wampe kura zao zote Tundu Lissu katika uchaguzio unaofuatiliwa kwa karibu na watanzania wa itikadi zote.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment