Monday, 6 March 2017

MAMA WA WATOTO WANNE WENYE ULEMAVU IRINGA ATAFUTA MSAADALUCY Amanyisye (katikati kwenye picha) mkazi wa Frelimo, mjini Iringa anaomba msaada wa hali na mali kutoka kwa wasamalia wema ili watoto wake wanne wenye ulemavu (aliokaa nao), waweze kupata matibabu na mahitaji yao mengine ya msingi.

Akizungumza kwa uchungu na hivikaribuni, Amanyasye aliwataja watoto hao kuwa ni Judith Luwanda (29), Cosmas Luwanda (25), Revocatus Luwanda (17) na Rosemary Luwanda (14).

Alisema watoto wake hao wana tatizo la akili (sio mtindio wa ubongo) ambalo halijaeleweka chanzo chake ni nini.

“Watoto wangu hawa wanne, wamesoma elimu ya msingi, lakini hawajui kusoma, kuhesabu wala kuandika chochote kile ikiwa ni pamoja na majina yao,” alisema mama huyo huku akitoa machozi.

Alipoulizwa kama wana uwezo wa kutofautisha thamani ya fedha (noti na sarafu) alisema hawajui na kila fedha wanayoiona wanaiita Sh 200. 

Kwa miaka 29 toka amzae mtoto wake wa kwanza Judith na wengine watatu baadaye, alisema maisha yake yaligeuka na kuwa ya kuwahangaikia watoto hao ili wapate matibabu ambayo pamoja na huduma za maombezi ya kiroho, hakuna mabadiliko yoyote waliyopata.

Alisema watoto hao wamekuwa wakishinda ndani, hawawezi kutumwa na wala kufanya shughuli yoyote kwa umakini unaotakiwa.

Alisema watoto hao wameifanya familia yao kuwa masikini, kwasababu sehemu kubwa ya fedha wanazopata zinaishia kuwahudumia watoto hao ambao hata hivyo wanasikia na wanaweza kujibu baadhi ya mambo.

Walipoomba na mwandishi wa habari hii kila mmoja aandike jina lake kwenye karatasi walilopewa, wote walishindwa na walipooneshwa noti ya Sh 10,000 na kuulizwa mmoja mmoja thamani yake, majibu yao yalikuwa Sh 200 na Sh 500.

“Naomba serikali na watanzania wanisaidie, bado naamini watoto wangu hawa wanaweza kufanyiwa uchunguzi mkubwa, wakapatiwa matibabu na kisha wakawa sawa na watu wengine,” alisema.

Alisema kwa yoyote atakayeguswa na tatizo la watoto hao anaweza kuwasiliana naye kwa simu 0754776229 na 0754778975  au akatuma msaada wowote kupitia akaunti yake ya  Lucy Amanyisye Malindo, namba 010-0025911 iliyopo benki ya Posta.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment