Monday, 6 March 2017

MAGUFULI AIONGEZEA MAKALI TANESCO

Rais, Dkt. John Pombe Magufuli.

Rais wa Jamhuri ya Munngano wa Tanzania Dkt, John Pombe Magufuli ametoa agizo kwa uongozi wa Shirika la Umeme Tanesco kukata umeme kwa Wizara au taasisi yoyote ya Serikali inayokwepa kulipa bili za umeme.

Rais Magufuli ameyasema hayo wakati akizindua na kuweka jiwe la msingi katika mradi wa umeme wa msongo wa Kv 132 Mtwara.

“Tanesco pasitokee taasisi ama Wizara hata Ikulu isipolipa umeme we kata tu, hatuwezi kujiendesha kwa hasara wakati kuna watu wanakwepa kulipia gharama wakati serikali inatoa ruzuku zake humu sasa ni wakati Tanesco ijiendeshe kwa faida,” amesema Rais Magufuli.


Aidha Rais Magufuli ameonya Tanesco kutoingia mikataba ya hovyo na makampuni ya nje yanayokuja kwa ujanja na kwamba kampuni ikitaka kuja kuwekeza umeme nchini basi waje wazalishe umeme wao na waiuzie Tanesco na wasitegemee umeme huu kufanya ujanja ili kutorudia mikataba mibovu kama symbion na makampuni mengine

Reactions:

0 comments:

Post a Comment