Monday, 20 March 2017

FREDERICK MWAKALEBELA AJITOSA UBUNGE WA AFRIKA MASHARIKI

Tokeo la picha la Fredeick Mwakalebela

ALIYEKUWA Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe, Frederick Mwakalebela amechukua fomu ya kuwani ubunge wa Bunge la Afrika Masharikia.

Mwakalebela ambaye ni kada maarufu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) alichukua fomu hiyo jana makao makuu ya CCM mjini Dodoma.

Akichukua fomu hiyo, Mwakalebela alisema alisema anawiwa kuwatumia watanzania kwa kupitia bunge hilo, kwa kuzingatia pia kwamba anazijua changamoto za Afrika Mashariki na watu wake.

“Uwezo wa kuwatumia watanzania kupitia bunge hili ninao na nazijua changamoto mbalimbali za Afrika Mashariki.” Alisema Mwakalebela ambaye pia liwahi kuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

“Nawaomba wabunge wanipe ridhaa nikawe mwakilishi wan chi hii katika bunge  hilo, nina imani CCM inanifahamu na hivyo itakuwa tayari kunituma ili niweze kuwatumikia,” alisema.

Aidha alimpongeza Mwenyekiti wa CCM Dk John Magufuli kwa kuunga mkono juhudi zake za kupambana na rushwa ndani ya chama hicho ili wapatikane viongozi wazuri na waadilifu.

Mwakalebela ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa alisema anao uzoefu wa uongozi wa kutosha na endapo atafanikiwa kuipata nafasi hiyo ahadi yake ni kutowaangusha watanzania.Reactions:

0 comments:

Post a Comment