Sunday, 19 March 2017

CUF YA MAALIM SEIF YAKUTANA ZANZIBAR

Tokeo la picha la CUF ZANZIBA

Leo tarehe 19 Machi, 2017 kutafanyika kikao cha kawaida cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama cha Wananchi (CUF)kitakachojadili masuala mbalimbali ya kitaifa, kiuchumi, kijamii na hali ya kisiasa nchini kwa ujumla.

Kikao hicho cha siku moja kilitanguliwa na kikao cha Kamati ya Utendaji ya Taifa kilichofanyika Jana tarehe 18 Machi, 2017 katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu iliyopo Vuga, Unguja na kuongozwa na Mwenyekiti wake Maalim Seif Sharif Hamad (Katibu Mkuu wa Chama).

Wajumbe wote Halali wapatao 53 wa kikao hicho kutoka pande zote mbili (Tanzania Bara na Zanzibar) wanatarajiwa kuhudhuria kikao hicho kitakachofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu Vuga, Unguja­Zanzibar, kikao kitafunguliwa rasmi na Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi Taifa Mheshimiwa Julius Mtatiro majira ya saa 4 asubuhi hii.

Pamoja na wajumbe wa Baraza Kuu pia wamealikwa katika kikao hiki wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Chama wote akiwemo Mzee Yohana Mbelwa, na Mwenyekiti wake Abdallah Khatau.

Kesho Jumatatu tarehe 20/3/2017 tutatoa maazimio ya kikao hicho kupitia Mkutano na waandishi wa habari.

CUF ni Taasisi Imara, yenye Viongozi Makini.
Haki Sawa Kwa Wote

Mbarala Maharagande

 Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi Na Mahusiano na Umma ­CUF TAIFA

Reactions:

0 comments:

Post a Comment