Monday, 20 March 2017

CHADEMA YATANGAZA MGOGORO NA MAKONDA

Tokeo la picha la freeman mbowe

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza rasmi kuwa na mgogoro na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na kumtaka Rais Magufuli kuchukua hatua dhidi ya kiongozi huyo.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kuwa chama chake kinatangaza kuwa mgogoro na Makonda kwa sababu hana sifa za kuongoza mkoa huo.

“Tunamtaka Rais Magufuli ajue kuwa CHADEMA tunatangaza rasmi mgogoro na Makonda. Hafai kuwa kiongozi katika ofisi yoyote ya umma,” amesema Mbowe.

Hivi karibuni Makonda amegonga vichwa vya habari na mitandao ya kijamii akishutumiwa kughushi vyeti vya kidato cha nne na kuingia katika malumbano na baadhi ya viongozi wa siasa na dini akiwemo Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima.


Pamoja na hayo kumekuwa na picha ya video inayosambaa katika mitandao ya kijamii ikimuonesha Makonda akiwa pamoja na askari wenye silaha wakivamia kituo cha redio na luninga cha Clouds Media na kuibua hisia tofauti miongoni mwa wanajamii huku uongozi wa Clouds ukiahidi kutolea ufafanuzi suala hilo.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment