Saturday, 11 March 2017

CCM YAWAFUKUZA VIGOGO 12, YUPO MWENYEKITI WA CCM MKOA WA IRINGA, DK JESCA MSAMBATAVANGU

Tokeo la picha la jesca msambatavangu

Chama cha Mapinduzi kimewafukuza makada 12 wa chama hicho akiwemo Mwenyekiti wa UMT na Mbunge wa Viti Maalumu Sophia Simba, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Ramadhan Madabida na Mwenyekiti wa Mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu.

Wengine waliofukuzwa ni pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara. Christopher Sanya na Mwenyekiti wa CCM Mkoa Shinyanga , Ernestr Kwirasa.

Wengine ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Madenge, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Assa Simba, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Ali Sumaye na Mjumbe wa NEC Arumeru, Mathiasa Manga.

Pia Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Longido, Leiza amefukuzwa uanachama pamoja na Mwenyekiti wa CCM Arusha Mjini, Saileli Mollel, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Gairo, Omary Hawadhi, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muleba, Babati na Bunda.

Wakati wanachama hao wakifukuzwa wengine wanne wamepewa onyo kali, sita wamevuliwa uongozi na kuwekwa chini ya uangalizi mkali wa miezi 30, huku mwenyekiti wa chama hicho Dodoma, Adam Kimbisa akisamehewa.


Uamuzi huo umetolewa baada wa kikao cha Nec kilichofanyika Dodoma leo (Jumamosi) na kuongozwa na mwenyekiti wake, Rais John Magufuli

Reactions:

0 comments:

Post a Comment