Thursday, 9 March 2017

BULEMBO KUBWAGA MANYANGA JUMUIYA YA WAZAZI CCM

Tokeo la picha la bulembo

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Abdallah Bulembo amesema kuwa hatagombea tena nafasi hiyo ya Uenyekiti wa Jumuiya hiyo katika uchaguzi ujao.

Bulembo ametoa kauli hiyo leo katika Kikao cha Baraza hilo Mjini Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine ametumia fursa hiyo kuwaaga wajumbe hao.

Amesema kuwa maamuzi hayo hayajatokana na Ubunge alioupata hivi karibuni baada ya kuteuliwa na Rais bali ni utaratibu wake aliojiwekea katika maisha yake.

 “Hoja hapa siyo ubunge kwamba nitakuwa na kofia mbili bali huu ni utaratibu wangu niliojiwekea katika maisha wa kutokung’ang’ania madaraka. Nilifanya hivi nilipokuwa Naibu Meya Musoma na nilipokuwa Kiongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Nchini (TFF),” amesema Bulembo.


Wakati huohuo, Bulembo amewaonya wajumbe wenye lengo la kuchukua fomu ili kumrithi kutomfuata wala kumpigia simu kutaka kuwasaidia na badala yake wafuate utaratibu wa jumuiya hiyo.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment