Wednesday, 22 March 2017

ASKOFU GWAJIMA ATOA POLE KWA CLOUDS

Tokeo la picha la Gwajima Clouds

ASKOFU wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Joseph Gwajima amezungumza na waandishi wa habari wa Clouds Media Group na kusema kilichomfanya afike katika ofisi hizo ni kutoa pole kwa kuwa yeye ni sehemu ya sababu za uvamizi huo.

“Isingekuwa busara watu wavamiwe na mimi ni mhusika mkuu halafu nisije kutoa pole,” alisema.

 Hatua ya Gwajima imekuja baada ya tukio la kituo hicho kuvamiwa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akiwa na polisi wenye silaha.


Gwajima amewasilia saa 4:00 asubuhi akiwa na msafara wa magari zaidi ya manne na walinzi wake takribani 30 na alipofika alipokelewa na Mkurugenzi wa vipindi na Uzalishaji Ruge Mutahaba.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment