Tuesday, 14 February 2017

UHAMIAJI WAMVAA YUSUPH MANJI

Tokeo la picha la YUSUPH MANJI

Ofisi ya Uhamiaji Jijini Dar es Salaam imemtaka Mfanyabiashara, Yusufu Manji kuripoti kwenye ofisi hizo baada ya kutoka hospitali alikolazwa.

Ofisa Habari wa Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam amedai kuwa Manji ameajiri watu wanaoishi nchini kinyume cha sheria.

Mfanyabiashara huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Yanga kwa sasa amelazwa katika Hospitali ya Muhimbili Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete baada ya kudaiwa kuzidiwa alipokuwa akihojiwa Kituo cha Polisi Kati kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya.Manji alifika kituoni hapo siku ya Alhamisi iliyopita kufuatia kuwa miongoni mwa watu 65 waliotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na kutakiwa kuripoti kituoni hapo siku ya Ijumaa iliyopita.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment