Thursday, 9 February 2017

TUNDU LISSU APANDISHWA KIZIMBANIMbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu

MBUNGE wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashitaka manne ya uchochozi.

Lissu amepandishwa kizimbani leo saa 6.25 mchana na kusomewa mashitaka hayo na wakili wa serikali Kishenyi Mutalemwa.

Mutalemwa alisema upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika lakini akawasilisha maombi ya kupinga dhamana ya mshatakiwa.

Katika maombi hayo amesema Lissu anakabiliwa na kesi nyingine tatu mahakamani hapo na kwamba ingawa yupo nje kwa dhamana amekuwa na mwenendo unaohatarisha amani kwa jamii na kwake mwenyewe kwa kuendelea kutoa maneno ya uchochezi.

Hata hivyo maombi hayo yalipingwa na wakili wa Lissu, Peter Kibatala akisema mashitaka yake yanadhaminika.Reactions:

0 comments:

Post a Comment