Tuesday, 28 February 2017

TUCTA YAWAKINGIA KIFUA WADAIWA WA BODI YA MIKOPO

Tokeo la picha la rais wa tucta

Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) limetoa siku 14 kwa Serikali kuwarejeshea wafanyakazi fedha za mikopo ya elimu ya juu wanazokatwa kimakosa vinginevyo watafanya uamuzi mgumu.

Hayo yamesemwa leo na Rais wa TUCTA, Tumaini Nyamhokwa na kudai kuwa wafanyakazi hao waliingia mkataba na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ya kukatwa asilimia nane (8) pekee.


 “Tunataka waliokopa kabla ya kupitishwa kwa sheria hii waendelee kukatwa asilimia nane na siyo 15 inayokatwa sasa,” amesema. Aidha, ameongeza kuwa baada ya sheria mpya iliyopitishwa Agosti, 2016 wafanyakazi sasa wanakatwa asilimia 15 bila kujali walikopa mikopo hiyo lini.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment