Sunday, 26 February 2017

RIDHIWANI KIKWETE KAANDIKA HAYA BAADA YA KUKUTANA NA EDWARD LOWASSA


Mbunge wa Chalinze (CCM) Ridhiwani Kikwete ambaye alikuwa miongoni mwa viongozi wa kisiasa waliohudhuria mechi ya Simba na Yanga katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam jana ametumia mtandao wake wa kijamii kueleza machache baada ya kukutana na aliyekuwa mgombea Urais kupitia Ukawa, Edward Lowassa.

Ridhiwani na viongozi wengine mashuhuri walikua wamekaa eneo la watu mashuhuri ‘V.I.P’.


Katika ukurasa wake wa Instagram Ridhiwani ameweka picha ya wawili hao na kuandika yafuatayo; “Siasa ni Shule ambayo haina mwisho. Nahisi bado niko shule ya Msingi na ninaendelea kujifunza, mimi ni kazi tu, Chalinze ni kazi tu, siasa si vita, tuhubiriupendo.”

Reactions:

0 comments:

Post a Comment