Tuesday, 14 February 2017

DAWA ZA KULEVYA ZAMTIA MBARONI ASKARI WA ARUSHA

Tokeo la picha la dawa za kulevya

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linawashikilia watuhumiwa 80 akiwemo askari polisi mmoja kwa tuhuma za kujihusisha na madawa ya kulevya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amesema hayo leo ofisini kwake na kudai kuwa hayo ni matokeo ya msako uliofanyika mwanzoni mwa mwezi huu na kufanikisha kukamata misokoto 3,845 ya bangi, kete 167 za Heroine na kilo 33 za mirungi.


Kamanda Mkumbo amesema miongoni mwa watuhumiwa hao, 40 ni wauzaji, msafirishaji 1, huku wengine 14 akiwemo askari polisi ni wale wanaojihusisha na biashara hiyo kwa njia moja ama nyingine.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment