Tuesday, 28 February 2017

CHADEMA WAIGEUKIA OFISI YA DPP

mahambowe

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeeleza kusikitishwa kwake na kitendo cha Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kunyimwa dhamana na kukaa gerezani kwa zaidi ya miezi minne sasa lakini pia wakaonyesha kuanza kuwa na imani na mahakama baada ya rufaa dhidi ya mbunge huyo kutupiliwa mbali.

Akiongea nje ya Mahakama Mjini Arusha, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema kitendo hicho kiliwafanya waichukie mahakama na kuona kuwa inapewa maelekezo na serikali, kumbe siyo kweli bali ni mchezo mchafu wa ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali (DPP).

“Mahakama imetufariji sana na kuturudishia imani yetu kwao kuwa ni chombo kilichosimama kwa miguu yake kama mhimili unaojitegemea na haipokei maagizo ya serikali,” amesema Mbowe.

Amesema sakata hilo linawasababisha kupeleka hoja katika bunge lijalo kuwa waangalie wafungwa na mahabusu waliomo ndani, kwani siyo wote waliokaa kwa sababu za kuhusika na makosa, bali wanaonewa.


Aidha amewapongeza majaji kwa kuitaka ofisi ya DPP kushikilia watu kwa misingi ya sheria na sio kuutia najisi mhimili huo kwa sababu ya michezo ya kisiasa.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment