Wednesday, 4 January 2017

KARIBU TENA HIFADHI YA TAIFA YA RUAHA


Hifadhi ya Ruaha iko katikati ya Tanzania umbali wa kilometa 128 magharibi ya mji wa Iringa. Hifadhi hii ina ukubwa wa kilometa za mraba 1300.

Hifadhi hii ni maarufu kwa wanyama aina ya kudu wakubwa na wadogo ambao hupatikana kwa wingi katika hifadhi. Ustawi wa hifadhi hii hutegemea kwa kiasi kukubwa mto Ruaha Mkuu.

Aina mbalimbali za samaki , viboko, na mamba hupatikana kwa wingi katika mto huu.

Wanyama kama pofu na swala pala hunywa maji katika mto huo ambao ni mawindo ya kudumu ya wanyama wakali kama simba, chui, mbweha na fisi.

Hifadhi hii inao idadi kubwa ya tembo wanaokusanyika katika eneo moja kuliko eneo lingine lolote Afrika Mashariki.

Hifadhi hii ina sifa ya kuwa na wanyama na mimea karibu yote inayopatikana kusini na mashariki mwa Afrika.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment