Tuesday, 17 January 2017

KAMATI YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI YAZURU MKOANI IRINGA


WAJUMBE wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, wamefanya ziara mkoani Iringa na kutembelea miradi mbalimbali ya umeme vijijini inayotekelezwa chini ya Wizara husika.

Kamati ilitembelea maeneo ya vijiji mbalimbali ambako miradi ya umeme vijijini imetekelezwa kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Awamu ya Pili.

Aidha, Kamati ilipata fursa kuzungumza na baadhi ya wananchi wa vijiji husika ambako miradi hiyo ya umeme inatekelezwa na kusikiliza maoni yao.


Baada ya ziara mkoani Iringa, Kamati hiyo itatembelea Mkoa wa Mbeya

Reactions:

0 comments:

Post a Comment