Wednesday, 14 December 2016

WAFUASI WA CUF WATWANGANA TENA

Tokeo la picha la wafuasi wa cuf watwangana

Wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF) kwa mara nyingine wametwangana  tena  makonde mahakamani.

Leo ni mara ya pili kwa wafuasi na wanachama wa chama hicho kutwangana makonde mahakamani wanapofika kusikiliza kesi inayozihusisha  pande  mbili  za  chama hicho.


Pande hizo ni  kati ya Mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa  na  Ofisi  ya  Msajili  wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba na upande wa Katibu Mkuu,  Maalim  Sharif Hamad.

Ugomvi huo umetokea mahakama kuu jijini Dar es Salaam leo ukiwahusisha walinzi wa viongozi  wa  chama hicho maarufu  kama mabaunsa wa  pande hizo  mbili umezimwa na askari polisi.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment