Tuesday, 6 December 2016

VIJIJI, KAYA ZOTE NCHINI KUWA NA UMEME IFIKAPO 2020

SERIKALI imeliagiza Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kujiandaa kusambaza wataalamu wake katika vijiji visivyo na umeme, watakaofanya usajili wa wananachi wanaotaka kuunganishwa na nishati hiyo.

Vijiji 7,873 kati ya vijiji 12,268  Tanzania Bara vinatarajiwa kuunganishwa na nishati ya umeme kupitia utekelezaji wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu unaofanywa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ndani ya miaka mitano.

Akizungumza na wananchi wa vijiji vya Sadani wilayani Mufindi na Ng’uruwe wilayani Kilolo kwa nyakati tofauti jana, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani ili mwananchi aweze kuunganisha umeme katika nyumba yake atalazimika kulipa Sh 27,000 tu.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment