Tuesday, 13 December 2016

TRUMP AMTEUA TILLERSON KUWA WAZIRI WA MAMBO YA NJE


Rais mteule nchini Marekani Donald Trump amethibitisha kuwa mkuu wa kampuni ya Exxon Mobil, Rex Tillerson ndiye waziri wa mambo ya nje nchini Marekani.

Bwana Trump alimsifu Tillerson mwenye umri wa miaka 64 kama mmoja wa viongozi wa biashara wenye tajriba kubwa zaidi duniani.

Bwana Tillerson anatajwa kuwa na uhusiano mwema na rais wa Urusi Vladimir Putin jambo ambalo limewatia wasiwasi wa wanademocrat na baadhi ya wa republican.


Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni nchini Marekani ndiye mwanadiplomasia wa cheo cha juu zaidi ambaye uhusika na sera za kigeni za nchi.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment