Sunday, 4 December 2016

RWAKATARE AKARIBISHA WATANZANIA KUOMBEA TAIFA

Tokeo la picha la mchungaji Rwakatare

MCHUNGAJI Getrude Rwakatare amesema katika  kuelekea  mwaka  mpya 2017 Watanzania mbalimbali wanakaribishwa katika kongamano la kufanya  maombi ya kuombea Amani Taifa katika kanisa hilo.

Rwakatere amesema hayo leo alipozungumza na waandishi  wa  habari  kuwa  kongamano hilo linaitwa ‘Shilo’ ni la sita kuanzia Desemba  4­11 ambapo litafanyika  katika kanisa hilo.

 Ameongeza kuwa kwa mwaka huu jumla ya watu kutoka  mikoa  24  watakusanyika kanisani hapo kwa siku nane kufanya maombi.


“Tutakayomuombea Rais, mawaziri na viongozi mbalimbali  bila  kusahau  amani ya nchi ambayo ni tunu tuliyoachiwa na waasisi wa Taifa hili,” amesema Mchungaji Rwakatare.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment