Tuesday, 13 December 2016

RONALDO AWA MCHEZAJI BORA WA DUNIA 2016

Cristiano Ronaldo na Lionel Messi kwa sasa wameshinda tuzo hii wakipokezana kwa miaka tisa mfululizo

Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amemshinda mpinzani wake Lionel Messi na kupata tuzo ya mchezaji bora wa dunia Ballon d'Or hii ikiwa ni kwa mara ya nne.

Ronaldo mwenye miaka 31 sasa anahitaji tuzo moja tu kumfikia Messi ambaye mwaka jana alipata tuzo ya tano.

Mshambuliaji wa Atletico Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa Antoine Griezmann amemaliza katika nafasi ya tatu.

Ronaldo aliisaidia Madrid kushinda ligi ya mabingwa ulaya msimu uliopita sambamba na kuisaidia nchi yake ya Ureno kushinda kombe la mataifa ya Ulaya 2016.

Kwa sasa ameshinda Ballon d'Or 2008, 2013, 2014 na 2016 na tokea mwaka 2009 amekuwa akipokezana na Messi.

''sikuwahi kuwaza kama ningeshinda Ballon d'Or mara nne'' nina furaha kubwa sana, najisikia fahari'' alisema Ronaldo.

''Natumia nafasi hii kuwashukuru wachezaji wenzangu, timu yangu ya taifa, makocha na watru wote walionisaidia kupata tuzo hii.'


Reactions:

0 comments:

Post a Comment