Sunday, 4 December 2016

KISWAGA AWAPIGA JEKI UVCCM IRINGA VIJIJINIMLEZI wa Chipukizi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa Iringa Vijijini, Jackson Kiswaga ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Tigo wa Nyanda za Juu Kusini ametoa msaada wa mizinga ya kisasa 10 ya kufugia nyuki kwa  Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wa wilaya hiyo.


Pamoja na kuwapatia mizinga hiyo itakayoweka katika kijiji cha Ilolompya Pawaga, Kiswaga amekubali ombi la umoja huo la kuwapatia fedha zitakazowawezesha kununua shamba la ukubwa wa ekari tano, wilayani Kilolo mkoani Iringa watakalopanda miti.

Mizinga hiyo ilipokelewa juzi na Katibu wa UVCCM Iringa Vijijini, Ignas Kinyoya aliyasema; “tunataka katika kipindi cha miaka mitano ijayo jumuiya yetu iondokane na sehemu kubwa ya ombaomba kwa ajili ya kufanikisha shughuli zake.”


Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Dodo Sambu ambaye pia ni mjumbe wa baraza kuu la jumuiya hiyo ya vijana alimshukuru Kiswaga kwa kuwajali vijana wa chama hicho huku akiwataka wadau wengine wa maendeleo waendelee kujitokeza kukiimarisha chama hicho.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment