Thursday, 1 December 2016

BOIMANDA MODERN CONSTRUCTION CO LTD- INATANGAZA NAFASI ZA KAZI ZIFUATAZO


INATANGAZA NAFASI ZA KAZI ZIFUATAZO

1.       MENEJA (Nafasi Mbili)
a.      Sifa
·        Awe tayari kufanya kazi hiyo katika kituo cha Njombe, Iringa au mahali pengine atakapopangiwa na mwajiri
·        Awe na shahada katika fani ya Uongozi, Utawala au Rasilimali Watu pamoja na elimu ya Biashara na Fedha
·        Awe na umri wa kati ya miaka 25 na 45, mwenye uzoefu wa kazi wa zaidi ya miaka miwili katika taasisi inayotambulika
·        Awe ni mbunifu, mpana katika uelewa wa masuala ya utawala na biashara, mchapa kazi na anayeweza kujisimamia
·        Awe na ufahamu wa kutosha kuhusu taratibu za uendeshaji wa makampuni
·        Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta pamoja na mifumo ya fedha katika kompyuta (Accounting packages)
·        Awe na uwezo wa usuluhishi (reconciliation attitude)

b.     Majukumu
·        Kumsaidia Mkurugenzi Mkuu wa kampuni kutekeleza majukumu ya kila siku ya kampuni
·        Kumshauri Mkurugenzi Mkuu kuhusu masuala yote yanayohusu wafanyakazi kwa upande wa utendaji kazi, maslahi na mahusiano kazini
·        Kusimamia na kuongoza shughuli zote za kampuni na kuhakikisha zinakwenda na kuendeshwa ipasavyo
·        Kuendeleza na kutekeleza mipango yote ya kampuni kwa kushirikiana na idara zake zote
·        Kutoa msaada wa kiutawala kwa kazi zote za kampuni na kuchukua hatua sahihi za kuboresha utendaji wa jumla wa kampuni
·        Kulinda mikataba na kusimamia mahusiano baina ya kampuni na wateja; na kusimamia utekelezaji wa majukumu ya watumishi wengine wote
·        Kuwasiliana na washauri na wakandarasi walioteuliwa na kampuni
·        Kuwasiliana na serikali na mamlaka zingine za kisheria
·        Kuandaa mipango kazi, ratiba za miradi, makadirio ya matumizi ya rasilimali na ripoti za utekelezaji wa miradi
·        Kufanya mikutano ya mradi, uchambuzi na ufuatiliaji
·        Kuwasiliana na vyombo na taasisi za fedha kuhusu usalama na usahihi wa rekodi za fedha za kampuni
·        Atakuwa msemaji wa kampuni akimsaidia Mkurugenzi Mkuu
·        Atawajibika kwa Mkurugenzi Mkuu na kufanya kazi yoyote ya kampuni kwa maelekezo ya kiongozi huyo


2.     MHASIBU MKUU (Nafasi mbili)
a.      Sifa
·        Awe tayari kufanya kazi katika mkoa wa Iringa , Njombe au katika kituo chochote atakachopangiwa na mwajiri.
·        Awe na shahada katika masomo ya uhasibu kutoka katika chuo chochote kinachotambuliwa na amesajiliwa na mamlaka za kisheria
·        Awe na ufahamu wa kutosha kuhusu taratibu, kanuni na sheria za makampuni
·        Awe na uzoefu ama uelewa wa kinadharia wa kukokotoa mizania ya mirejesho ya kodi za makampuni kwa mujibu wa kanuni na taratibu za TRA
·        Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta pamoja na mifumo ya fedha katika kompyuta (Accounting packages)
·        Awe mbunifu, mwaminifu, anayejituma na anayeweza kujisimamia mwenyewe
·        Awe na uzoefu wa kazi hii wa kipindi kisichopungua miaka miwili
·        Awe na umri wa kati ya miaka 25 na 45

b.     Majukumu
·        Ndiye atakayehidhinisha hati za malipo kwa maelekezo na kwa kuzingatia taratibu za kampuni
·        Ataandaa taarifa ya mapato na matumizi ya mwezi
·        Atasimamia wahasibu wasaidizi katika kazi zao za kila siku
·        Atasimamia shughuli za uhasibu kwenye kitengo cha Idara
·        Ataandika taarifa ya maduhuli
·        Kutayarisha ripoti maalumu ya fedha kwa kukusanya, kuchambua na kufupisha maelezo ya akaunti
·        Awe na uwezo wa kukokotoa mizania ya mirejesho ya kodi za makampuni kwa mujibu wa kanuni na taratibu za TRA
·        Atahakikisha malipo kwa wafanyakazi na vyama vingine yanafanywa kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu kwa kufuata miongozo na sera ya kampuni
·        Atachambua mwenendo wa mapato na matumizi ya kampuni na kupendekeza viwango vya bajeti vinavyokwenda sambamba na udhibiti wa matumizi
·        Kufanya kazi nyingine zozote kwa maelekezo ya manejimenti

3.      MHASIBU MSAIDIZI (Nafasi mbili)
a.      Sifa
·        Awe tayari kufanya kazi ama katika mkoa wa Iringa, Njombe au katika kituo chochote atakachopangiwa na mwajiri
·        Awe na stashahada (diploma) katika masomo ya uhasibu
·        Awe na ufahamu wa kutosha kuhusu utaratibu, kanuni na sheria za makampuni
·        Awe mbunifu, mwaminifu, anayejituma na anayeweza kujisimamia mwenyewe
·        Awe na umri wa kati ya miaka 25 na 45 na uzoefu wa kazi usiopungua miaka miwili
·        Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta pamoja na mifumo ya fedha katika kompyuta (Accounting packages)

b.     Majukumu
·        Awe na uwezo wa kupokea na kulipa fedha
·        Ajue namna ya kutunza daftari la fedha
·        Ajue kufanya usuluhishi wa hesabu za benki
·        Ajue kukagua hati za malipo
·        Ajue kupitisha malipo kulingana na kanuni za fedha
·        Ajue namna ya kusimamia kazi za wasaidizi wa hesabu
·        Atakuwa msaidizi wa mhasibu mkuu

4.     AFISA UGAVI
a.      Sifa
·        Awe na shahada au stashahada ya juu katika fani ya manunuzi na ugavi (materials management) kutoka katika chuo kinachotambuliwa na serikali
·        Awe na cheti cha CPSP na awe amesajiliwa na PSPTB na uzoefu wa kazi usiopungua miaka miwili
·        Awe na umri wa kati ya miaka 25 na 45
·        Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta pamoja na mifumo ya fedha katika kompyuta (Accounting packages)
·        Awe na uzoefu wa kazi usiopungua miaka miwili

b.     Majukumu
·        Atatakiwa kutambua mahitaji ya bidhaa na huduma mbalimbali za kampuni na kufanya manunuzi kwa wakati muafaka na kwa gharama nafuu kwa kuzingatia sheria ya manunuzi na kanuni zake
·        Kuwashauri viongozi wa kampuni kuhusu kanuni na taratibu sahihi za kufuata wakati wa kufanya manunuzi ya bidhaa na huduma kwa ajili ya kampuni
·        Kwa kusaidiana na viongozi wa kampuni kuweka kumbukumbu ya vifaa vilivyo chakaa, ambavyo havijachakaa na thamani yake
·        Kuandaa makabrasha ya tenda, na kupokea na kuwasilisha tenda
·        Kuhakikisha nyaraka zote za ununuzi na uuzaji zinapatikana na kujazwa vizuri kwa kuzingatia sheria na kanuni za ununuzi
·        Kuhakikisha kwamba nyaraka zote za ununuzi na uuzaji zinatunzwa vizuri kwa ajili ya kumbukumbu pale zinapohitajika
·        Atafanya kazi nyingine zozote kwa maelekezo ya manejimenti


5.      AFISA KUMBUKUMBU (nafasi mbili Njombe na Iringa)
a.      Sifa
·        Awe na shahada ya kwanza katika fani ya utunzaji na uhifadhi wa kumbukumbu (records managements & archives) kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na serikali
·        Awe na umri wa kati ya miaka 25 na 45
·        Awe na uzoefu wa kazi usiopungua miaka miwili
·        Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta na mifumo yake ya uhifadhi wa kumbukumbu


b.     Majukumu ya kazi
·        Kudhibiti mifumo ya kumbukumbu, kutunza na kusimamia matumizi ya kumbukumbu za kampuni
·        Kutambua na kutafuta kumbukumbu katika masijala za kampuni
·        Kudhibiti mfumo wa kumbukumbu zinazozalishwa na kompyuta, na kutunza na kusimamia matumizi yake.
·        Kufanya kazi nyingine atakayopangiwa.

Mwisho wa kupokea maombi ya kazi hizi ni Desemba 31, 2016

Maombi yote yatumwe kwa njia ya Posta kwa


Mkurugenzi Mkuu,
Boimanda Modern Construction Company Ltd,
S.L.P 1491,
Iringa.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment