Wednesday, 12 October 2016

MKUTANO WA NICOL WAZUIAWA

Tokeo la picha la felix mosha

JESHI la Polisi limezuia mkutano wa dharura wa Wananchama wa Kampuni ya Uwekezaji ya Nicol uliokuwa umekwisha andaliwa kufanyika katika Ukumbi wa Karimjee.

Polisi leo waliingilia kati na kumwamuru, Felix Mosha ambaye anadai kuwa yeye ni Mwenyekiti wa Nicol kuusitisha mkutano huo mara moja.

Mkutano huo umezuiwa kufanyika baada ya jeshi hilo la polisi kupitia nyaraka mbalimbali za kiserikali, Mahakama Kuu, Mahakama ya Biashara na Mahakama ya Rufaa hususani katika hukumu zilizotolewa katika kesi ya madai namba 16 ya 2011 pamoja na kesi ya biashara namba 288 ya 2014.

Kwenye kesi hizo, Nicol ilikuwa ikiwakilishwa na wakili wa kujitegemea kutoka kampuni ya uwakili ya BM, Benjamin Mwakagamba.

Katika hukumu zote hizo, zimethibitisha uhalali wa maamuzi ya wanahisa katika kikao kilichokaa Aprili 14,2012 ambacho kilimuondoa madarakani Felix Mosha ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Kampuni hiyo ya uwekezaji ya Nicol.

Katika kutolewa kwa maelezo hayo, Mosha alishauriwa kusubiri maamuzi ya rufaa namba 24 ya mwaka 2016 ambayo aliikata yeye mwenyewe katika Mahakama ya Rufaa.


Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala, Salum Amdani amesema ni kweli wameuzuia mkutano huo kufanyika kwa sababu kuna shauri linaloendelea katika Mahakama ya Rufaa.  

Reactions:

0 comments:

Post a Comment