Saturday, 29 October 2016

DC KILOLO AIPIGA JEKI PANAMA GIRLS FC YA MJINI IRINGA
TIMU ya soka ya wanawake ya mjini Iringa inayoshiriki Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara ya Panama Girls , imepigwa jeki kwa kupewa vifaa mbalimbali vitakavyoiwezesha kushiriki ligi hiyo.

Vifaa hivyo ambavyo ni pamoja na seti moja ya jezi kwa wachezaji 18, makocha na viongozi wa timu hiyo, soksi, vifaa vya golikipa na sabuni vimetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Asiah Abdallah.

Naye Mbunge wa Viti Maalumu wa Mkoa wa Iringa, Ritha Kabati (CCM) ametoa Sh 50,000 kuichangia timu hiyo

Reactions:

0 comments:

Post a Comment