Saturday, 29 October 2016

ACT WAMKINGIA KIFUA ZITTO KABWE

Tokeo la picha la Zitto Kabwe

Chama cha ACT­ Wazalendo kimefungua milango kukaribisha uchunguzi juu ya mali na madeni ya kiongozi wake mkuu Zitto Kabwe.

Akizungumza na waandishi wa habari Katibu wa Kamati  ya  Bunge  na  Serikali  za  Mitaa  ya  ACT,  Habib Mchange alisema chama hicho hakina shaka kwamba kiongozi wake ni msafi.

"Tunavitaka vyombo vya uchunguzi vianze kazi hiyo  mara  moja na  tutafurahi  ukihusisha  pia  akaunti zake binafsi "alisema Mchange.

Mtandao wa Jamii Forum umeripoti haya…. 

AFANDE SELLE AMLIPUA ZZK

Leo katika kundi la "Tanzania 2015 & Beyond" ambalo lina wabunge, mawaziri, maprofesa, wanasiasa na wanazuoni wa nje na ndani ya nchi (nami ni member pia) kumeibuka mjadala juu ya ufisadi wa NSSF ukimhusisha Zitto Kabwe na chama cha ACT wazalendo na baadhi ya viongozi waandamizi wa chama hicho.

Moja ya tuhuma hizo ni pamoja na NSSF kununua shamba la ekari moja kwa Shilingi milioni 800 katika mazingira yenye utata maana shamba hilo linakadiriwa kuwa na thamani ya milioni 10 tu.

Lakini ZZK pamoja viongozi wenzie wa ACT wamekuwa wakiitetea NSSF kwa muda mrefu kuwa haina ufisadi. ZZK akiwa mwenyekiti wa wa kamati ya hesabu za mashirika ya umma amekua akiisifia na kuitetea bungeni kwa nguvu zote na kusema ripoti zao za fedha ni safi.

Halikadhalika gazeti la ACT liitwalo "MwanaHabari" limekua likitumika kuisafisha NSSF na kusifia baadhi ya miradi yake yenye harufu ya ufisadi.

Sasa leo mwanachama wa ACT na mgombea Ubunge wa Morogoro mjini kupitia ACT Ndg Selemani Msindi (Afande Selle) ametoa maoni yake kuhusiana na chama chake cha ACT na kashfa za NSSF.
________________

Afande Selle anasema;

Nje ya uvyama kila Mtanzania Mzalendo anahitaji majibu ktk hili kwani kulingana na tetesi za muda mrefu kutoka kwa watu tofauti ni kwamba hata uanzishwaji wa chama chetu cha ACT ni matokeo ya matunda ya ufisadi huo mkubwa uliotendeka ndani ya NSSF ikiwa ni malengo maalum ya kuvuruga upinzani imara uliokuwepo wkt wa uchaguz mkuu na si kujenga chama/taasisi imara ya ACT..

Lengo kuu lilikuwa ni kujipendekeza kwa serekali mpya ya chama tawala kama ilivyokua ktk serikali iliyopita ya JK ambayo kupitia serikali ile uswahiba wa kiongoz wa chama chetu na mkurugenzi wa NSSF ulishamiri kupita kawaida huku upigaji wa kutisha ukitamalaki.

Lkn bahati mbaya malengo hayo hayakufanikiwa wkt wa uchaguz kwa ACT kushindwa kwa aibu ktk ngazi zote hali iliyopelekea serekali mpya kuona haina sababu ya kuibeba ACT au viongozi wake kwani haitovuna chochote na ndipo JPM pamoja na kumsifu ZZK kipindi kile aliposalia bungeni peke yake baada ya wapinzani wote kutoka nje ya bunge lkn akamtosa kwa mambo mengine tofaut JK aliyewabeba ZZK na Mr. Dau.

Hapo ndipo hasira za ZZK zikawaka na kuanza kuwa mkosoaji mkubwa wa JPM binafsi na serekali yake... Anafanya hivyo si kwa sababu ya uzalendo wake kwa nchi bali kwa sababu maslahi yake binafsi yameguswa.. 'Kweli itatuweka huru... Wacha party ianze http://emoji.tapatalk-cdn.com/emoji447.png ...niendele ama nisiendeleeee..

Seleman Mshindi (Afande Sele)

Mwanachama wa ACT WAZALENDO na Mgombea ubunge Morogoro Mjini 2015(ACT).


Reactions:

0 comments:

Post a Comment