Tuesday, 13 September 2016

ZUMA ASALIMU AMRI NA KULIPA FEDHA ZA UMMA ALIZOTUMUA KUKARABATI NYUMBA YAKE

Tokeo la picha la jacob zuma

RAIS Jacob Zuma wa Afrika Kusini hatimaye amelipa deni la Dola za Marekani 509,000 sawa na zaidi ya Sh Bilioni Moja ikiwa ni fedha za umma alizozitumia kukarabati nyumba yake binafsi.

Wizara ya fedha nchini humo ilikuwa imependekeza kuwa Rais Zuma alihitajika kurejesha fedha hizo 509,000 serikalini zilizotumiwa kukarabati nyumba yake huko Nkandla.

Zuma aliifanyia maboresho nyumba yake kwa vitu vya gharama likiwamo bwawa la kuogelea na kituo cha wageni akidai alikuwa anaimarisha usalama.

Machi mahakama ya katiba ilitoa hukumu kwamba rais huyo alishindwa kutekeleza katiba.

Kashfa zinazomgusa Zuma zimeleta athari kubwa katika siasa ndani ya chama chake cha ANC ambapo katika uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika hivi karibuni, kilipoteza majiji makubwa katika historia ya chama hicho.


Chama kikuu cha upinzani cha Democratic Alliance katika tamko lake, kimepongeza uamuzi wa Zuma kulipa deni lake lakini kikasema hiyo ni hatua ndogo katika kashfa za rushwa anazokabiliana nazo.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment