Wednesday, 7 September 2016

ZITTO AISHANGAA SERIKALI YA AWAMU YA TANO

Tokeo la picha la zitto kabwe

Chama cha ACT­Wazalendo kimelaani kwa nguvu zote hatua ya Serikali ya CCM kuvunja Katiba ya nchi na kujaribu kuweka pembeni utawala wa sheria.

Kiongozi wa ACT­Wazalendo, Zitto Kabwe amesema Serikali ya CCM imeamua kutumia nguvu ya polisi kuzuia shughuli za kisiasa.

Amesema kwa hali ilivyo sasa, kwa mujibu wa Serikali ya CCM, shughuli za kiuenezi za vyama vya siasa kama mikutano ya hadhara na maandamano na mikutano ya ndani vilipaswa kukoma baada ya Uchaguzi Mkuu.

“Kisheria, huu ni uvunjifu wa Katiba na sheria za nchi. Kisiasa tunatambua viongozi wa CCM wamepoteza mvuto kwa wananchi. Kutokana na hili wameamua kumtumia mwenyekiti wao (Rais John Magufuli) kutumia polisi kuokoa taswira ya chama chao mbele ya umma,” alisema Zitto.


Zitto alikuwa anazungumzia hatua za hivi karibuni zilizochukuliwa na Kamishna wa Polisi wa Operesheni na Mafunzo, Nsato Marijani ambaye alipiga marufuku mikutano na maandamano kwa sababu mbalimbali ikiwamo uvunjifu wa amani

Reactions:

0 comments:

Post a Comment