Monday, 5 September 2016

WATUHUMIWA WA MAUAJI YA DADAKE BILIONEA MSUYA WAONGEZEKAMarehemu Aneth Msuya .

Idadi ya washtakiwa katika kesi ya mauaji ya Aneth Msuya ambaye alikuwa dada wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu wa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro, Ersato Msuya maarufu kwa jina la Bilione Msuya, imeongezeka na kufikia wawili.

Awali, Agosti 23, mwaka huu mshtakiwa Miriam Mrita (41) ambaye ni mke wa bilionea huyo alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa shtaka la mauaji ya Aneth aliyekuwa wifi yake.

Hata hivyo, juma moja baadaye, mfanyabiashara wa jijini Arusha, Revocatus Evarist (40), alipandishwa kizimbani katika Mahakama hiyo na kuuunganishwa na Miriam kwenye kesi hiyo.


 Evarist alipandishwa kizimbani mahakamani hapo Ijumaa iliyopita na kusomewa shtaka la mauaji ya Aneth na Wakili wa Serikali, Diana Lukondo.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment