Tuesday, 13 September 2016

WABUNGE WAKUBALI KUKATWA POSHO KUCHANGIA MAAFA KAGERA

Tokeo la picha la bunge la tanzania

WABUNGE wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wameunga mkono juhudi za serikali na wameridhia kukatwa posho ya siku moja ili kuchangia waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea Kagera.

Hatua hiyo inafuatia muongozo wa mbunge wa Mlalo CCM, Rashid Shangazi aliyeomba kiti kutoa muongozo ili wabunge watoe fedha hizo kama sehemu ya kuomboleza pamoja na waathirika.

Hoja hiyo iliungwa mkono na wabunge wa pande zote bila kuangalia itikadi zao. H√Ęta hivyo,Mbunge wa Tarime vijijini Chadema John Heche alisema chama chake kilishatoa Sh 100,000 kila mbunge lakini kufuatia hoja hiyo na wao wapo tayari kuchangia posho zao.

Wakati huo huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa George Simbachawene amesema madaktari bingwa zaidi ya 15 kutoka Mwanza wamepelekwa Kagera kwa ajili ya kuongeza huduma kwenye hospitali.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment