Monday, 5 September 2016

TRA YAIMARISHA UKUSANYAJI KODI KARIAKOO

Tokeo la picha la kariakoo

KILA MFANYABIASHARA katika eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam atalazimika kuwa na Mashine ya Kielekroniki ya Kodi (EFDs) baada ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kulitangaza eneo hilo kuwa Mkoa Maalumu wa Kodi.

Mkakati huo unalenga kuongeza wigo wa vyanzo vya kukusanya mapato kikamilifu.

TRA imechukua uamuzi huo kwa kigezo cha Kariakoo kuwa kitovu cha biashara nchini.

Kutokana na uamuzi huo, mamlaka hiyo imeagiza kila mfanyabiashara wa eneo hilo kumiliki Mashine ya Kielektroniki ya Kodi (EFDs).


Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi TRA, Richard Kayombo alisema katika kutekeleza hilo mawakala wote wa EFDs wamefungua ofisi ya pamoja jengo la Al­Falah lililopo Mtaa wa Msimbazi.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment