Sunday, 4 September 2016

SERIKALI YATAKIWA KULINDA WANAHABARI, MASLAI YAO

Tokeo la picha la jane mihanji

SERIKALI imeombwa kulinda na kutetea mazingira ya ufanyaji kazi kwa wanahabari ili kukuza na kuboresha taaluma hiyo kwa maslai na taifa kwa ujumla.

Endapo serikali itafanya hayo, imeelezwa, jamii itapata taarifa sahihi za mienendo mbalimbali ikiwamo masuala ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Akizungumza katika kumbukumbu ya miaka minne ya kifo cha mwanahabari Daudi Mwangosi, Makamu wa Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Jane Mihanji alisema kuna haja kwa serikali kuwalinda wanahabari.


Mkurugenzi wa UTPC, Abubakar Karsan alisema umoja huo unalaani vikali vitendo vibaya wanavyofanyiwa wanahabari nchini.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment