Monday, 26 September 2016

SERIKALI YAJA NA SHERIA YA KUPANDIKIZA VIUNGO

securedownload

Serikali kupitia Wizara ya Afya na Hospitali ya Muhimbili (MNH) ipo katika mchakato wa mwisho wa maandalizi ya sheria ya upandikizaji wa viungo baada ya kutumia sheria ya kimataifa ya mwaka 2011 kwa muda mrefu.

Maandalizi hayo yanalenga kuanza kutoa huduma ya upandikizaji wa figo ifikapo Januari, 2017.

Huduma hiyo inatarajiwa kuanza kutolewa baada ya MNH kupatiwa mkopo wa shilingi bilioni 3.7 kutoka Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa (NHIF) kwa ajili ya kutengeneza vyumba sita vya upasuajia ili kufikia 19 na kununua vifaa kwa ajili ya upasuaji wa figo, lakini pia kufanya ukarabati wa hospitali hiyo.

Mkurugenzi wa Tiba wa Muhimbili, Dkt. Hedwiga Swai amesema awali Tanzania haikuwa na sheria ya upandikizaji wa viungo ambao hujumuisha upandikizaji wa ini na figo.

“MNH tukishirikiana na Wizara tutatengeneza na tutaiwasilisha kwa wizara na wao wataipitisha katika mchakato ndipo ianze kutumika na sasa ipo ianze kutumika na sasa ipo katika hatua za mwisho,” amesema.

Licha ya maandalizi ya sheria hiyo, Dkt. Swai amesisitiza kuwa itakapokamilika itaelezea mchakato mrefu utakaotumia kuchangia figo na nani anaruhusiwa kuchagia.


“Kutakuwa na viapo, vyeti vya kuzaliwa, uthibitisho wa ndugu, bodi ambayo inakubali upandikizaji husika, na vilevile kutakuwa na mratibu wa upandikizaji,” ameongeza.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment